Dalali Smart

Karibu kwenye Mfumo Wako Mpya wa Kupata Nyumba za Kupanga Tanzania!

Je, unatafuta nyumba ya kupanga? Unahitaji duka au ofisi kwa ajili ya biashara yako? Au labda una nyumba, chumba au jengo la kupangisha?

Karibu kwenye mfumo mpya kabisa, uliobuniwa na vijana wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia jamii yetu kupata makazi kwa urahisi, haraka na kwa uwazi mkubwa

Unatafuta? Tunakusaidia!

Kupitia mfumo wetu, unaweza:

  • Kutafuta nyumba za kupanga kulingana na mahitaji yako (eneo, bei, ukubwa n.k.)

  • Kupata maduka au majengo ya kibiashara

  • Kuunganishwa moja kwa moja na wamiliki wa nyumba au mawakala walioaminika

  • Kuweka alert ili tukutaarifu mara tu nyumba inayokufaa inapotokea!

Unapangisha? Tunakuunganisha na wapangaji!

Kama wewe ni mmiliki wa nyumba au jengo, unaweza:

  • Kupakia taarifa za nyumba zako kwa urahisi kabisa

  • Kupata wapangaji waliothibitishwa na wenye nia ya kweli

  • Kufuatilia maombi, mawasiliano na miamala yote kwa usalama

Muunganiko wa Moja kwa Moja

Mfumo wetu si tu kutafuta na kupangisha — ni mahali ambapo wahitaji na wapangishaji hukutana moja kwa moja. Hakuna usumbufu, hakuna ulaghai. Kila kitu kiko wazi, salama, na rahisi kutumia

Ni Rahisi Kuanza

  1. Tembelea tovuti yetu / app

  2. Jisajili kama mpangaji au mpangishaji

  3. Anza kutafuta au kupakia nyumba zako

  4. Wasiliana na wapangaji au wamiliki kwa urahisi

Huduma kwa Wateja

Tuna timu ya msaada inayopatikana muda wote kukusaidia. Unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia WhatsApp, simu au barua pepe. Tupo kwa ajili yako!

Hii ni huduma kwa jamii – kutoka kwa vijana, kwa ajili ya Watanzania wote.

Tuungane pamoja kuleta mapinduzi ya makazi Tanzania. Hakuna tena kulipia madalali wasioaminika. Hakuna tena kuhangaika mtaani bila mafanikio.

about image